.....................................
Na Said Hauni, Lindi.
CHAMA cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha
Ilulu SACCO'S Manispaa ya
Lindi,kimekopesha kwa wanachama 442 kati ya 672 mikopo yenye thamani ya
Sh,726,500,000 ikiwemo ya kilimo kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Mwenyekiti wa Chama hicho Yusufu Nadeng'u ameeleza hayo alipokuwa anawasilisha
taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi hicho katika mkutano mkuu wa 17
uliofanyika mjini Lindi.
Akiwasilisha taarifa yake hiyo, Nadeng'u amesema
mikopo hiyo imehusisha shughuli za kilimo,vyombo vya usafiri,vikundi na vikundi
vya wajasiliamali imetolewa Disemba 17/2022 hadi Disemba 16 mwaka huu.
Alisema mikopo iliyotolewa wapo wafanyabiashara
wa kati na wadogo,wanachama wanaojihusha na kilimo,wajasilimali na waendesha
pikipiki na kufanya jumla ni Sh,726,500,000.
Mwenyekiti huyo amewaeleza wajumbe wa mkutano huo
Sh,94,500,000/= zimetolewa kwa waendesha pikipiki,sh,35,400,000, kilimo
Sh,12,600,000 vikundi vya wajasiriamali na Sh,15,250,000 zilizobaki zimeenda
kwa wafanyabiashara wadogo na wakati.
Alisema kati ya mikopo uliokopeshwa jumla ya
sh,614,200,157/_zimeanza kurejeshwa na kufanya kiasi kilichobaki mikononi mws
waliokopeshwa ni sh,107,112,842.
Nadeng'u alisema licha ya mafanikio
hayo,bado chama kina madeni sugu yenye
thamani ya sh,20,885,222/_kati ya hizo baadhi ya wanachama wameweza kurejesha
kwenye chama Sh 8,120,120/_na kufanya kiasi kilichosalia ni sh,22,765,102.
"Pamoja na changamoto zilizopo baadhi ya
wanachama wetu kutorejesha kwa wakati mikopo wanayochukuwa chama kimeendelea
kupata faida, "alisema Nadeng'u.
Alisema katika kipindi hicho chama kimeweza
kuongeza idadi ya wanachama kutoka 621 hadi 672 sanjari na kupata cheti na tuzo
bora Mkoa wa Lindi mwaka 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza na wanachama hao wa Ilulu SACCO'S amewataka waendelee kuwa wamoja kwa kuwapa ushirikiano mzuri kwa maendeleo ya chama chao.








No comments:
Post a Comment