MWENYEKITI AMCOS URAMBO, AKAMATWA KWA MADAI YA UBADHIRIFU - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, May 11, 2024

MWENYEKITI AMCOS URAMBO, AKAMATWA KWA MADAI YA UBADHIRIFU

Mkuu  wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,  Elibariki Bajuta akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa AMCOS ya Magulungu hivi karibuni wilayani humo.

.........................

Na Nyamizi Moses,  Urambo, Tabora

MKUU wa Wilaya ya Urambo Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,  Elibariki Bajuta amewasimamisha kazi na  kuwakamata baadhi ya wajumbe na Mwenyekiti wa bodi ya AMCOS ya Magulungu Kata ya Muungano kwa madai ya ubadhirifu wa fedha za wananchama wa AMCOS.

Haya yametokea hivi karibuni baada ya Mkuu wa Wilaya kufika katika AMCOS ya Magulungu ambapo wanachama wa AMCOS wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu wakidai fedha zao kwa viongozi bila kupata majibu yanayoeleweka kutoka kwa bodi hiyo.

Katika kikao hicho viongozi wametuhumiwa kwa upotevu wa fedha za wananchama zaidi ya Sh. Milioni  80 hatua iliyopelekea Kamishna Bajuta kuagiza kukamatwa kwa viongozi hao na kuagiza Jeshi la Polisi kuanza uchunguzi kwa kushirikiana na Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kubaini kama kuna upotevu wa fedha hizo zinazolalamikiwa.

Hata hivyo Kamishna Bajuta amesema serikali haipo tayari kuendelea na baadhi ya Viongozi ambao wanakwamisha maendeleo ya wananchi.

Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano na mkuu wa wilaya ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Usikivu ukitawala katika mkutano huo.
Mkutano ukifanyika.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad