Kijana Lucas Mhambo ambaye inadaiwa alitekwa na kukatwa miguu na mikono na watekaji akisaidiwa wakati akitoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa ambapo Serikali imetoa ahadi ya kumunulia viungo bandia.
............................
Na Mwandishi, Wetu Kilosa.
SERIKALI imesema itampatia Viungo Bandia kijana Lucas Mhambo mwenye umri wa
miaka 24 mkazi wa Dumila Wilaya kilosa ambaye amepata ulemavu wa kudumu baada
ya kutekwa na watu wanaodaiwa kuwa vibaka na alipofikishwa hospitali
ililazimika kukatwa miguu na mikono yote Ili kuokoa uhai wake.
Akizungumza ofisini kwake Wilayani Kilosa, Mkuu wa Wilaya ya hiyo Shaka Hamdu Shaka amesema baada ya kupata changamoto ya kijana huyo serikali ya Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan itagharamia gharama za ununuzi
wa Viungo bandia Ili kimuwezesha kumudu majukumu yake ya
kawaida hasa katika kufanya shuhuli ndogo ndogo za kujipatia kipato na kuweza
kujikimu na familia yake.
"Inasikitisha sana na tunaendelea kulaani vikali vitendo hivi vya
ukatili dhidi ya binadamu ambavyo vinadumaza shuhuli za mtu moja moja katika
kupambania maisha, kitendo hiki kimeua ndoto za ndugu yetu hivyo Serikali ya
Dkt Samia Suluhu Hassan itahakikisha tunamsaidia kupata viuongo hivyo bandia
ili aweze kujisaidia" alisema Shaka.
Shaka ameleeza kuwa Serikali itaendelea kujali na kuhudumia wananchi
wote wenye changamoto mbali mbali hivyo
itamsaidia kijana huyo ili aweze kufanya shughuli ambazo zinaweza kumuingizia
kipato kwa vile tayari anayo familia inayomtegemea kama baba.
"Gharama za viungo bandia pamoja na matibabu ni T. Shs, Milioni 15
tukumbuke hana mikono wote miwili na miguu yote miwili, niendelee kuwasili
watanzania wenye moyo wa kumsaidia waendeleee kufanya hivyo kwani bado
anahitaji msaada wa hali na Mali" alisema Shaka.
Kwa Upande wake Lucas Mhambo anasema tukio Hilo lilitokea
Oktoba 14 mwaka 2023 baada ya mtu mmoja kuja eneo lake la kazi (bodaboda )
akiomba apelekwe Kijiji jirani, njiani waliongezeka na kumkaba kisha kumfunga
kamba miguu ,mikono huku mdomoni wakimfunga kitambaa na kumtupa msituni ambapo
alionekana na raia wema baada ya siku tatu kupita.
Amefahamisha kuwa baada ya Siku ya
tatu kupita na wasamalia wema alifikishwa hospital kwa ajili ya kupatiwa
matibabu lakini nilibanika viungo hivyo vimeharibika na haiwezi kutibika zaidi
ya kukatwa vyote ambapo hadi sasa anaishi na ulemavu huo.
Hata hivyo Lucas amewashkuru
watanzania wote waliojitolea kipindi chote cha matibabu yake akiwa
hospital ya Taifa Muhimbili na akiwa nyumba ambapo michango hiyo imemuwezesha
kufanya huduma za matibabu kuwa nyepesi na kuanzia kuanzia maisha.
"Namshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa
kuguswa na changamoto hizi kunishika
mkono, watanzania wote waliojitolea kunisaidia mungu atawalipa zaidi walichotoa
kwangu bado nahitaji msaada wao napitia magumu mno na kwa atakaeguswa anaweza
kunisaidia kupitia Acc No 22710017881 Adam khalfa NMB Bank. Simu 0717382021" Amefafanua Lucas huku machozi yakimwagika.
Pamoja na kuwa serikali itamchangia matibabu na kununua viungo bandia imebainika
kuwa na bado kijana Lucas anahitaji kununua kiti mwendo na kujenga nyumba
ambayo amefikia hatua ya kupaua sambamba
na changamoto ya fedha za kurejea hospitali kila baada ya siku Tano Ili kusafisha vidonda
ambavyo anaendelea kujiuguza.










No comments:
Post a Comment