MSD YAKABIDHI DAWA KWA MFUMO WA KIELEKITRONIKI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, July 4, 2024

MSD YAKABIDHI DAWA KWA MFUMO WA KIELEKITRONIKI

Meneja wa Bohari ya Dawa  (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa (katikati) akiwa na Afisa Huduma Mwandamizi kwa Wateja MSD Kanda ya Kati, Juliana Mbogo (kulia) pamoja na Msimamizi wa ujenzi wa ghara la kisasa la kuhifadhia dawa linalojengwa Dodoma, George Emmanuel (kushoto) wakati wa kwenda kuona ujenzi wa ghara hilo unavyoendelea.

----------------------------------

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza kukabidhi dawa kwa wateja wake kwa kutumia mfumo wa kielekitroniki hatua ambayo imerahisisha namna ya kufanya makabidhiano hayo.

Hayo yamebainishwa Julai 3, 2024 na Meneja wa Bohari ya Dawa  (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea MSD Kanda hiyo kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo Kanda ya Dodoma.

“MSD tumeanza kukabidhi dawa katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwa mfumo wa Kielekitroniki na mfumo huo unafanywa kupitia dereva ambaye anakwenda kukabidhi mzigo huo kwa kutumia simu yake ya mkononi,” alisema Jumaa.

Jumaa alisema dawa hizo zinapokabidhiwa kwenye Hospitali  au kituo cha afya inashirikishwa kamati ya afya ya kijiji au kitongoji husika na kufuata taratibu zote zilizowekwa.

Aidha waandishi hao wakiwa kanda hiyo ya MSD waliweza kutembelea ghara kubwa la kisasa la kuhifadhia dawa pamoja na kwenda kuona ujenzi wa maghara mengine  yanayojengwa karibu na eneo la ofisi ya MSD Kanda ya Dodoma.

Kwa Upande wake Afisa Huduma Mwandamizi kwa Wateja MSD Kanda ya Kati, Juliana Mbogo, alisema kanda hiyo inahudumia Mikoa miwili ya Dodona na Singida ambapo kwa Singida inahudumia halmashauri saba huku Dodoma ikiwa Halmashauri 8 na Wilaya ya Kiteto  ambayo ina halmashauri moja.

Mbogo alisema mkoa huo wa Dodoma MSD imepewa jukumu la kuhifadhi dawa na kuzisambaza.

Safari ya kwenda kujionea ujenzi wa ghara hilo ukiendelea.

Msimamizi wa ujenzi wa ghara, George Emmanuel akielekeza hatua ya ujenzi wa ghara hilo ulipofikia.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai (katikati) na Meneja wa Bohari ya Dawa  (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa wakitoka kuliangalia ghara hilo.
Afisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka na Meneja wa Bohari ya Dawa  (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa wakiwa tayari kwa safari ya kukagua ujenzi wa ghara hilo.
Waandishi hao wakichukua taarifa za ujenzi wa ghara hilo.
 Wanahabari wakitoka baada ya kukagua.Muonekano wa maghara hayo .
--AGALIA VIDEO--

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad