........................................
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama
ameuhakikishia umma wa wanaruvuma kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya
itaendele na uboreshaji wa huduma za Afya ikiwemo upatikanji wa vifaa, vifaa
tiba pamoja na dawa.
Waziri Mhagama amesema hayo Septemba 20, 2024 baada ya kuwasili mkoani
Ruvuma na kupokelewa na Mkuu wa mkoa huo Mhe. Ahmed Abbas.
Waziri Mhagama amesema Mkoa huo wa Ruvuma utanufaika na ujenzi wa wodi
maalum za watoto wachanga waliozaliwa na uzito pungufu (NCU) ili kufikia lengo
la Serikali kupunguza vifo vya watoto.
Kuhusu suala la lishe, Waziri Mhagama amesema Serikali inaendelea na zoezi
la kutoa elimu kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ambao katika kila Kitongoji
watakua Wawili (Wakike na Wakiume) watakaotoa elimu na huduma za kijamii za
awali kwa wananchi.
Ziara ya Waziri Mhagama mkoani Ruvuma inafanyika siku chache kabla ya ziara
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
itakayoanza Septemba 23 mkoani humo.
Waziri Mhagama akiwa mkoani Ruvuma anatarajia kutembelea miradi mbalimbali
inayotekelezwa katika Jimbo la Peramiho ikiwemo kukagua utoaji wa huduma kwenye
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (RRH), Kukagua utekelezaji wa mradi mpya
(New OPD) pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Sekta ya Afya.








No comments:
Post a Comment