Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito, akizungumza na waandishi wa habari Septemba 27, 2025 Jijini Tanga.
...........................................
Na Mashaka Kibaya,Tanga
MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo amesema, ifikapo oktoba 29 mwaka huu ni muhimu kwa kila mwananchi kwenda kupiga kura huku akiasa kuwapuuza wale waliopo nje ya nchi aliowaeleza kuwa na malengo ya kuharibu amani ya nchi.
Mbali na hayo,Gombo amesema pindi akiingia madarakani,katika kipindi cha siku 100 za uongozi wake anaanzisha mchakato wa katiba mpya sanjari na kushughulukia changamoto ya upatikanaji ajira kwa watu wenye sifa ili kuziba pengo lililopo katika wakati uliopo.
Gombo ameyasema hayo jana (Leo) katika mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Tanga,ambapo alisema watanzania wanapaswa kuachana na dhana potofu akiwasihi kuona umuhimu wa kwenda kupiga kura.
Alitoa wito huo ikiwa sehemu ya kujibu awali aliloulizwa kuhusiana na msimamo wa CUF ambapo alisema,taarifa za makatazo hata yeye amekuwa akizisikia kupitia mitandao ya kijamii 'social media' na kwamba wanaozioneza wako nje ya nchi huku akisema ni wale wasiokuwa na nia njema.
"Hizi taarifa ninazisikia kwenye 'social media", Watanzania waache dhana potofu siku ikifika wakapige kura tusisikilize wale waliopo nje ya nchi ambao wanataka kuvuruga amani, kama wana nia njema nawaje tupambane pamoja"alisema Gombo.
Kuhusu mapokeo waliyopata kutoka kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ambayo CUF imefanya mikutano yake,bGombo alisema kuwa, ameshuhudia mafanikio makubwa kwa Wananchi kupokea vizuri sera za Chama Cha Wananchi (CUF).
"Tunatarajia mambo yatakuwa mazuri kwa muitukio tulioupata, wananchi wamepokea vizuri sera zetu mfano matibabu bure,elimu na hata ajira kwa wenye sifa" alisema mgombea huyo wa kiti cha urais kupitia tiketi ya CUF.
Mambo mengine ambayo Gombo aliahidi kuyayekeleza pindi akiingia madarakani ni, kuhakikisha huduma za Serikali zinatolewa ngazi ya kata huku akifuta kikokotoo sanjari na sheria ya utumishi wa umma ikiangaliwa upya.
Gombo amewaomba watanzania kumchagua ili kukiwezesha Chama Cha Wananchi CUF kushika dola huku akiwaasa kutoionea huruma CCM akileza kuwa chama hicho kimeshindwa kuwatumikia Wananchi.
Mgombea huyo wa urais aliongeza kusema kuwa, katika maboresho anayokusudia kwenye sekta ya elimu, ni kutokuwepo kwa mikopo ya elimu ya juu na badala yake elimu hiyo itatolewa bure.
Wakati kampeni za uchaguzi zikiendelea nchini kwa wagombea kunadi sera zao amevisihi vyombo vya dola kutokubali kutumika, amesema ni vyema vikatenda haki kwa wote huku akitoa ushauri kwa tume ya uchaguzi kufanya kazi zake kikamilifu kwa kuhakikisha hakuna mgongano wa ratiba kwenye mikutano







No comments:
Post a Comment