RUWASA KILINDI KUTUMIA ZAIDI YA SH.BILIONI 2 KUBORESHA MIRADI YA MAJI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, 29 January 2026

RUWASA KILINDI KUTUMIA ZAIDI YA SH.BILIONI 2 KUBORESHA MIRADI YA MAJI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, Michael Chabai akiongoza kikao cha baraza la madiwani. Kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa.

..........................

Na Mashaka Kibaya,Kilindi.

KATIKA kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini wilayani Kilindi mkoani Tanga, Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh. Bilioni 2.5 kwa kipindi cha robo ya pili mwaka 2025/2026.

Hayo yamo kwenye taarifa ya Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wilayani humo Mhandisi Philipo Bajuta, aliyoitoa Januaari 28, 2026 kwenye baraza la Madiwani na kueleza kuwa fedha hizo ni za ukamilishaji,uboreshaji, utafutaji vyanzo na ujenzi wa miradi ya maji.

Bajuta alisema Sh. 903,365,983,.87 ni fedha za lipa kwa matokeo (PforR), Sh.1,150,911,544.36 ni fedha za mfuko wa maji (NWF), Sh. 500,000,000 ni fedha kutoka Serikali kuu (GoT).


Alisema Ruwasa Wilaya ya Kilindi, inakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa barabara zake unaosababishwa na mifugo, imeshauri wananchi kuendelea kuelimishwa ili kusaidia kutunza miundombinu hiyo kwa kutopitisha wanyama barabarani.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilayani humo, Mhandisi Martin Mwashambwa, akitoa taarifa ya matengenezo ya barabara kwa kipindi cha robo ya pili Septemba hadi Disemba 2023-2024,2024-2025 na 2025-2026 alisema, TARURA inakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa barabara unaosababishwa na mifugo hali inayotokana na uwepo wa mifugo mingi, na ili kutatua changamoto wananchi wanapaswa kuelimishwa kuona umuhimu wa kutumia njia mbadala kupitisha mifugo yao.

"Wakala wa barabara Mjini na Vijijini TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi inakabiliwa na changamoto ya uharibifu unaosababishwa na mifugo, utatuzi wa changamoto hii ni kuendelea kuwaelimisha wananchi kuona umuhimu wa kutunza barabara na miundombinu yake kwa kutopitisha mifugo barabarani badala yake kupita kwenye njia mbadala"alisema Mwashambwa.

Changamoto nyingine amezitaja kuwa ni jiografia ya Wilaya ya Kilindi ambayo imefanya barabara nyingi kupita kwenye milima na mabonde makubwa hivyo kuhitaji matengenezo makubwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja.

Ili kutatua changamoto hiyo ,Mwashambwa alisema, inahitajika kuendelea kuomba fedha kutoka vyanzo vingine mbali na mfuko wa barabara kuweza kutatua kero za baadhi ya barabara zinazohitaji matengenezo makubwa sambamba na ujenzi wa madaraja.

"Utatuzi wa changamoto hii ni kuendelea kuomba fedha kutoka vyanzo vingine vya fedha mbali na mfuko wa barabara, mwaka huu Serikali imeongeza fedha za Jimbo Shilingi Bilioni moja na ongezeko la bajeti kupitia tozo za mafuta shilingi bilioni mbili"alisema.

Changamoto nyingine ni ile ya kutokuwepo kwa fedha za dharura za kufanyika matengenezo ya haraka pindi barabara hizo zinapoharibiwa na mvua ambapo suluhisho lake ni kutengwa fedha za dharura kwa kipindi cha mvua.

Pia kuna changamoto ya uhaba wa maeneo ya kuchimba changatawe kwa ajili ya ujenzi wa barabara  ambapo utatuzi wake ni vijiji kutenga maeneo ya kuchimba malighafi hiyo wakati wanapoandaa mipango yao ya matumizi bora ya ardhi.

Kuhusu utekelezaji wa miradi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mwashambwa alisema, kufikia mwaka wa fedha 2023/2024 robo ya pili 2025/2026 Disemba 31, 2025 wamepokea shilingi 818,401,115.8 kutoka mfuko wa barabara ambazo ni kati ya Sh.980,113,478.26 zilizopangwa.

Alisema,fedha za mfuko wa jimbo zilizotengwa kwa matengenezo ya barabara mwaka wa fedha 2023/24 ni Sh.500,000,000 wakati kiasi cha fedha kilichopokelewa ni shilingi 332,760,000 ambazo ni sawa na asilimia 66.55 ya bajeti inayotokana na fedha za Jimbo.

Aidha, alisema kuna nyongeza ya bajeti ya Sh.1,000,000,000 bilioni inayotokana na tozo imetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara na kiasi cha fedha kilichopokelewa ni shilingi 755,340,645.00 sawa na asilimia 75.53% ya bajeti yote iliyoyengwa kutokana na fedha za tozo.

Kuhusu matengenezo ya barabara, Mwashambwa alisema,kufikia Disemba 2025 robo ya pili 2025/2026 Mwaka wa fedha 2023 wameendelea kufanya matengenezo ya kawaida ambapo kati ya jumla ya Km 9.36 zilizokuwa kwenye mpango wa matengenezo Km 8.01 zimelimwa na Sh.22,880,000 zimelipwa kati ya Sh.129,190,000 zilizotengwa.
 

Alisema pia kumefanyika matengenezo ya sehemu korofi, kati ya jumla ya Km 13.50 zilizokuwa kwenye mpango zimelimwa na kiasi cha fedha zilizolipwa ni shilingi 63,710,415.00 kati ya shilingi 292,500,000.00 zilizotengwa sawa na asilimia 21.7.

Vile vile yamefanyika matengenezo ya muda maalum ambapo Km 19.8 zimelimwa na shilingi 63,015,000.00 kulipwa kati ya shilingi 290,780,000.00 na kwenye ujenzi wa madaraja box culvert 24 na drift 4 vimejengwa ambapo Sh.167,000,000.00 zimelipwa kati ya Sh.167,000,000 zilizotengwa.

Madiwani wakiwaa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilindi, Mhandsi Philip Bajuta. akizungumza.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilindi, Mhaaandisi Martin Mwashambwa, akitoa taarifa ya matengenezo ya barabara.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad