Je, kuna uchungu kama wa kufanya kazi kwa bidii halafu ukaonekana kama haupo? Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Benson, mfanyakazi wa kampuni ya vifaa vya ujenzi jijini Nairobi, ambaye kwa miaka miwili alijituma bila kupandishwa cheo wala kuongezewa mshahara.
Benson alikuwa mfanyakazi wa kuaminika. Hakuwahi kuchelewa. Alikubali kufanya kazi hata wikendi bila malipo ya ziada. Lakini kila alipothubutu kuomba nyongeza, aliambiwa asubiri. Mara ya kwanza aliambiwa kampuni inapitia changamoto. Mara ya pili akaambiwa bado hajafikia vigezo. Mara ya tatu aliambiwa kuna watu wengi zaidi wanahitaji nafasi hiyo.
Alianza kukata tamaa.








No comments:
Post a Comment