Mwanaume mmoja jijini Dar es Salaam alipata mshtuko wa maisha yake baada ya kuleta mpango wa kando nyumbani kwake wakati mkewe akiwa amesafiri kwenda kijijini. Mara tu walipolala kitandani tayari kwa “michezo”, ghafla kitanda kiligeuka kuwa kama bwawa la maji makuu na mwanaume huyo akaanza kuzama huku akipiga kelele za kuomba msaada.
Yule mwanamke aliyekuja naye aliona kitanda kimejaa nyoka wakubwa na akakimbia nje uchi wa mnyama huku akipiga kelele za “Mwizi! Mwizi!”. Majirani walipofika, walimkuta mwanaume huyo akipapatika sakafuni akidai anazama, ingawa chumba kilikuwa kikavu.








No comments:
Post a Comment