Naitwa Theresia, mwanamke ambaye kwa miaka
mingi nimeishi nikiwa na hofu kubwa ya kuitwa “mwanamke wa mikosi.” Kwa nje
nilikuwa naonekana mrembo, mwenye mvuto na kila sifa ya kuitwa mke, lakini
nyuma ya pazia kulikuwa na giza nene ambalo lilikula furaha yangu kwa zaidi ya
miaka kumi na miwili.
Kila mwanaume aliyekuwa akijitokeza na kutaka
kunioa, alikuwa anakumbwa na balaa kubwa. Wa kwanza alipata ajali mbaya wiki
mbili kabla ya harusi, wa pili alipoteza kazi yake ghafla na akachanganyikiwa,
na wa tatu alihama nchi bila kutoa taarifa yoyote punde tu baada ya kutoa posa.








No comments:
Post a Comment