Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akitoa maagizo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA) kuhakikisha wanaweka mkakati wa kuimarisha mitaji ikiwa ni sehemu ya mchango wa Dira 2050, wakati wa kikao na uongozi wa Mamlaka hiyo, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba.
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akisikiliza maelezo ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati wa kikao na Uongozi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA), kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA), Bw. Lucas Mwimo, akizungumza kuhusu ongezeko la wawekezaji katika soko hilo, wakati wa kikao na Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (hayupo pichani), kilichofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Dionisia Mjema, akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) na Uongozi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA), kilichofanyika katika Ofisi Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba.
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA), Bw. Lucas Mwimo, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (wa tatu kutoka kulia), Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, (wa pili kulia) na wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA), Bw. Lucas Mwimo (wa pili kushoto), baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
-----------------------------------------
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameiagiza Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA) kuendelea kutoa elimu ya masuala ya uwekezaji kwa wanachi ili waweze kuwekeza kwa faida.
Mhe. Balozi Omar, alitoa maagizo hayo wakati wa kikao chake na uongozi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA) kilichofanyika Ofisi za Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Alisistiza kuwa elimu ya uwekezaji ni nyenzo muhimu ya kuwasaidia Watanzania kuelewa fursa zilizopo na namna ya kuzitumia kwa manufaa ya kiuchumi.
“uwekezaji sahihi kupitia masoko ya mitaji unachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa taifa” Alisema Mhe. Balozi Omar.
Aliipongeza Mamlaka ya CMSA kwa ukuaji wa thamani ya uwekezaji kwa asilimia 128 ambapo kwa mwaka 2021 kulikuwa na ukuaji wa shilingi trilioni 28 na hivi sasa ukuaji huo umefikia shilingi trilioni 65.2.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA), Bw. Lucas Mwimo, alimhakikishia Mhe. Waziri kuwa Bodi yake itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.
Alisema kuwa, Bodi ya CMSA inatambua umuhimu wa elimu ya uwekezaji na itaongeza ushirikiano na wadau mbalimbali ili kufanikisha azma ya Serikali ya kukuza uchumi wa wananchi.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama, alisema kuwa wamepiga hatua kubwa katika kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye masoko ya mitaji.
“Tulikuwa tunaendelea na zoezi la kutoa elimu na kampeni za uhamasishaji ambalo limechangia ongezeko la washiriki wapya, ambapo Watanzania wengi sasa wanajitokeza kuwekeza kwa njia rasmi na salama”, alifafanua Bw. Mkama.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Dionisia Mjema.
No comments:
Post a Comment