Anamiliki maduka ya mapambo ya ndani baada ya msoto mkali!
Naitwa Said, mkazi wa jiji la Dar es Salaam, maeneo ya Kariakoo mtaa wa Congo. Kwa miaka tisa, nimekuwa nikihangaika na biashara ya kuuza mazulia, mapazia, na mashuka ya gharama. Kila mmoja anajua kuwa Kariakoo ndiyo moyo wa biashara, hivyo niliwekeza mamilioni ya pesa niliyopata baada ya kustaafu kazi yangu ya ulinzi.
Lakini ndugu zangu, nilichoambulia ni maumivu ya mgongo kwa kukunjua na kutandika mazulia kila asubuhi huku hakuna mteja anayenunua hata kitambaa cha meza.
Hali hii ilikuwa inanidhalilisha sana, hasa ukizingatia kuwa mimi ni mtu mzima mwenye familia inayonitegemea. Nilikuwa nafika dukani saa kumi na mbili asubuhi, lakini saa kumi na mbili jioni inafika sijaingiza hata shilingi mia tano.
Mazulia yangu yalianza kufubaa rangi kwa kupigwa na vumbi la barabarani, na panya walianza kutafuna pindo za mashuka yangu.








No comments:
Post a Comment