Naitwa Martha, mkazi wa mkoa wa Dodoma. Mimi ni mjasiriamali na nimejikita katika ufugaji wa kuku wa nyama na mayai kwa miaka mitano sasa. Ufugaji huu ndio umeniwezesha kujitegemea na kusaidia ndugu zangu kijijini. Nilikuwa na banda kubwa lenye kuku 500 ambao walikuwa wamefikia muda wa kuuzwa. Nilikuwa nimeshapata soko katika hoteli kubwa za hapa mjini, na nilikuwa nasubiri siku ya kesho yake kuanza kusambaza kuku hao ili nipate fedha za kuanza mradi mwingine wa ufugaji wa mbuzi.
Hata hivyo, usiku wa kuamkia siku ya mauzo, wezi walivamia banda langu. Walitumia mbinu za kuwapulizia kuku dawa ili wasipige kelele, kisha wakawasomba kuku wote 500 kwa kutumia lori dogo. Asubuhi nilipoenda bandani kuwapa chakula, niliwakuta walinzi wakiwa wamelala fofofo na kuku wote hawapo. Nilihisi kama damu imekauka mwilini.








No comments:
Post a Comment