Naitwa Brenda, mkazi wa jijini Arusha. Kazi yangu ni kuratibu na kupamba sherehe za harusi (Wedding Planner). Kwa miaka kumi, nimekuwa nikiwaingiza mamia ya maharusi ukumbini kwa mbwembwe na bashasha, lakini moyoni nilikuwa na kidonda kikubwa.
Kila nikimaliza kupamba harusi ya mtu na kurudi kwangu usiku, nilikuwa nalia kwa uchungu nikijiuliza, “Lini itakuwa zamu yangu?”
Licha ya urembo wangu na uwezo wangu mkubwa wa kifedha, wanaume walikuwa wakinikimbia kama vile mimi ni ugonjwa wa mlipuko. Kila niliyeanzisha naye mahusiano, alikuwa anakaa mwezi mmoja na kusema, “Brenda, wewe ni mzuri sana lakini sipo tayari kwa ndoa,” kisha baada ya wiki mbili namuona anaoa mwanamke mwingine. Nilihisi nina nuksi inayovutia wanaume wa “kupitisha muda” tu lakini siyo wa kufunga pingu za maisha.








No comments:
Post a Comment