MUNGEREJA ACHAGULIWA ASKOFU MKUU WA KWANZA GETHSEMANE - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, 28 March 2026

MUNGEREJA ACHAGULIWA ASKOFU MKUU WA KWANZA GETHSEMANE

    Askofu Mkuu wa Kanisa la Gethsemane, Ariel Mungereja (katikati), kushoto ni Katibu mkuu Abel Ajema na kulia ni makamu askofu, Baita Momba.

.................................

Na Mwandishi Wetu. 

WAUMINI wa Kanisa la Gethsemane temple Assemblies Tanzania, wamemchagua Ariel Mungereja kuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini. 

Mungereja anakuwa askofu wa kwanza wa kanisa hilo, baada ya uchaguzi mkuu wa kikatiba uliofanyika Machi 27, mwaka huu.

Uchaguzi ambao ulikuwa wa kwanza tangu kanisa hilo, lisajiliwe na Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania Agosti 15, 2025, ulifanyika katika Makao Makuu ya kanisa hilo, yaliyopo Kinyerezi, Kichangani, jijini Dar es Salaam. 

 Katika uchaguzi huo, uliosimamiwa na mwenyekiti wa muda, Adam Butiti alimtangaza Mungereja kuwa askofu mkuu baada ya kupata kura 50 za ndiyo huku tatu zikimkataa, kati ya kura 53 zilizopigwa na waumini wa kanisa hilo.

Pia, Butiti alimtangaza Baita Momba kuwa Makamu Askofu wa kanisa hilo Tanzania baada ya kupata kura 50 za ndiyo huku kura tatu za hapana. 

Katika uchaguzi huo, Abel Ajema alichaguliwa nafasi ya katibu mkuu baada ya kupata kura 53 zote za ndiyo huku Ambakise Hosea akitangazwa mshindi katika nafasi ya mweka hazina kwa kupata kura 53 zote za ndiyo. 

Viongozi wengine waliochaguliwa ni Butiti ambaye ataiongoza bodi ya wadhamini akiwa mwenyekiti, ambapo Festo Mwakalebela alichaguliwa katika nafasi ya ukatibu mkuu, Christina Bundo, Shilinde Buzinde, Antony Sandawe wajumbe wa bodi hiyo. 

Wengine waliochaguliwa katika nafasi ya kamati ya nidhamu ni Neema Ambakisye, Simon Ole Makumbale na Butiti. 

Kwa mujibu wa katibu ya kanisa hilo, viongozi hao watatumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad