Naitwa Elias, mkazi wa zamani wa maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam. Kwa zaidi ya miaka minane, nilikuwa nikijishughulisha na ufundi wa simu na kuuza vifaa vidogo vidogo pembezoni mwa barabara. Licha ya kuwa na utaalamu wa hali ya juu, maisha yangu yalikuwa ni dhoruba tupu.
Nilikuwa nafika kazini asubuhi na mapema, lakini jua lilikuwa linazama bila mteja hata mmoja kuingiza simu kwangu. Nilikuwa naishia kushindia jojo na maji ili kuficha njaa, huku nikiona wenzangu wakipata dili za maana.
Hali hii ilinifanya nianze kujichukia. Nilijiona kama mwanaume aliyelaaniwa kwa sababu kila nikijaribu kuweka akiba ili nikuze biashara, dharura za ajabu zilikuwa zinatokea na kuitafuna ile pesa yote. Nilihisi kuna ukuta wa chuma uliozuia riziki zangu usoni.








No comments:
Post a Comment