
NA MAGENDELA HAMISI, KARATU ARUSHAWAKULIMA zmkoani Arusha ambao wamepata mafunzo ya kuendesha Kilimo Ikolojia wameonesha kwa vitendo kwamba Tanzania inaweza kuachana na matumizi ya viwatilifu na mbolea za kiwandani.Kwa mujibu wa George Ndege ambaye ni miongoni mwa wakulima wa Kilimo Ikolojia, Karatu mkoani Arusha anabainisha kwamba Kilimo Ikolojia ambacho kinatumia pembejeo asili, zisizo za viwandani kimekuwa na faida kubwa kiafya kwa walaji na ulinzi wa ardhi kulingana na mabadiliko ya tabia nchi.Mzee Ndege, anasema katika eneo lake la ekari 10 amekuwa akilima mboga mbonga, kahawa na ufugaji nyuki na anabaisha kwa kwamba mboga anazolima zimekuwa zikihitajika zaidi kutokana kwamba ni bora zaidi kuliko zile zinazokuzwa kupitia mbolea za viwandani. “Hapa kwangu nalima mbogamboga, kahawa kwa kutumia mbolea samadi na madawa ya asili kwa kuzitengeza mwenyewe na kufanya kuwa salama zaidi kwa mlaji tofauti na zile zinazokuzwa kwa viwatilifu na mbolea za viwandani.Anasema soko lake kubwa baada ya kuvuna ni katika hoteli za kitalii zilizoko Karatu mkoani Arusha na zimempa mafanikio lukuki ikiwemo kumuongezea kipato na kujenga baadhi ya nyumba za kulala wageni hapo Karatu.Pia anabainisha kwamba amekuwa na uhakika wa soko ingawa anashindwa kutoleza kwa maana mahitaji ni makubwa kwani kwa sasa anahudumia hoteli tano tu licha ya kuwepo hoteli za kitalii zaidi ya 80 katika viunga hivyoNaye, Mzee Modest Fantee, mkulima kutoka kijiji cha Endagem, Karatu mkoani Arusha ameweka wazi kwamba kupitia kilimo Ikolojia amekuwa akipata mazao lukuki bila kutumia kilimo kinacholeta athari katika ardhi.Elimu ya Kilimo Ikolojia nimeipata kutoka taasisi ya IDP, ambayo imekuwa msaada mkubwa kwetu kwani wanatupatia mbegu za asili na kutunzishia mfumo wa kuweka benki za mbegu vijijni na hapa kwangu nina benki ya mbegu na zinalindwa kwa njia ya asili.“Kwa kutumia kilimo Ikolojia hata familia yangu inakuwa na chakula cha kutosha chenye lishe bora kutokana ukuaji wake haukuwa wa viwatilifu vyenye kemikali, hapa natumia mbolea ya ng’ombe na viwatilifu vya asili ninavyotengeneza mwenyewe.“Nashukuru pia baada ya sisi kuanza kutumia za Kilimo Ikolojia, tumeanza pia kuwafundisha wengi na kwetu tumekuwa kama darasa, hivyo elimu hii inaendelea kusambaa maeneo mengine ndani ya Kata yetu na nje,” amesema.Pia, Adili Msangi ambaye anajishulisha na kilimo Ikolojia pamoja, ufugaji, utengenezaji wa mbole hai na viwatilifu vya asili na uhifadhi wa mbegu asili, wilayani Karatu, anakili kuwa kutumia mifumo ya kilimo endelevu, imewasaidia kuwa na uzalishaji wa mazao salama kwa matumizi ya binadamu na utunzaji wa mazingira.Kwakweli Kilimo Ikolojia kimetusaidia kutupa matokeo mazuri katika ardhi kwa kupata mazao salama kwani tunatumia mbolea asili zinzotengenezwa kwa mifupa ya wanyama, pamoja na mabaki ya mazao ambayo kwa wengine wanaona ni takataka nasi tunazibadilisha na kuwa kitendea kazi na kutupa matokeo mazuri shambani. “Aidha tunatumia mkojo wa ng’ombe ambao tunauvundika na mwisho wa siku unakuwa ni kiwatilifu na hiyo imekuwa ikivutia wakulima wengi kujia kufunza na kwenda kuitumia kwao na kuachana na viwatilifu vyenye kemilikali.“Tunatumia viwatilifu na mbolea za asili lengo ni kuhakikisha tunapata mazao salama kwa matumizi ya binadamu lakini pia kilimo Ikolojia hakiui wadudu bali kinafukuza lakini ukitumia za viwandani vinaua wadudu wote wakiwemo wale wanaopevusha mazoa wakiwemo nyuki na vipepeo, amesema. Amesema tangu apete elimu ya kilimo Ikolojia mwaka 2017 hadi sasa amekuwa na mafanikio makubwa shambani na wigo mpana wa kusambaza mbegu asili kwa wakulima wengine ingawa changamoto kubwa anayopata ni ukosefu wa mashine ya uchakataji mifupa kwa ajili ya kutengeneza mbole inayogharimu milioni 12.













No comments:
Post a Comment